Karibu katika blog yetu tanze safari ya kufanikiwa na kuwa na uhuru wa kifedha
Alhamisi, 20 Oktoba 2016
Faida Tano za Kuacha Kufuga kwa Mazoea.
Karibuni tena Wafugaji tuendelee na safari yetu ya matumaini, siku ya leo tutaangazia faida tano muhimu tutakazopata kama tukiondokana kabisa na desturi ya kufuga kwa mazoea, kama tulivyokwisha soma katika makala zilizotangulia, nimeongelea mara kwa mara juu ya jambo hili, nalionglea sana jambo hili kwa sababu limewafikisha wafugaji wengi pale walipo sasa hivi ninapoandika makala haya, hali ya wafugaji wengi inafahamika jinsi ilivyo, hakuna faida inayoonekana kinyume na matarajio ya walio wengi.
Jamii nyingi za wafugaji wamekuwa watumwa wa jambo hili, kwamba jinsi yao ya kufuga imekuwa ile ile tangia enzi za mababu na mababu .Fahari yao kubwa ikiwa ni kuwa na kundi la mifugo mingi kadri inavyowezekana .Hapa tunaona kubwa linalopatikana ni sifa isiyokuwa na faida yoyote, kwamba, Mzee fulani hapa kijijini ndiye Tajiri namba moja, ana ng'ombe Elfu tano, mbuzi elifu mbili na kondoo miatano.
Sasa angalia maisha ya huyu Mzee, mavazi yake anayovaa ni yale yale miaka yote, kipande cha lubega chafu, viatu vya matairi ya gari na fimbo mkononi. Kazi yake ni kuamka asubuhi na mapema na kuanza kuswaga mifugo yake kutwa nzima kusaka malisho popote yanapoweza kupatikana, iwe ni sehemu halali au vinginevyo, ilimradi mifugo yake ipate chakula.
Zoezi hili siyo la mchezo, safari ya kusaka chakula inaweza kuwa hata ya miezi kadhaa bila ya kurejea nyumani, sasa hapo hata uangalizi wa familia unakuwa wa mashaka sana kwani hata mambo ya watoto kupata elimu yanakuwa siyo ya msingi sana au hata hayafikiriwi achiliambali kupewa kipaumbele. Kumbuka hapa tulikuwa tunaangazi juu ya wafugaji wa jamii kubwa ya wafugaji.
Kwa wafugaji wa kawaida tunaofuga kwa uchache iwe mjini au mashambani, nasi hatutofautiani sana na jami ya wafugaji wakubwa, tendo lile lile la kufuga kwa mazoea na ufugaji usiokuwa na tija uko pale pale! kwamba tunakuwa na idadi ya wanyama ambao bajeti ya kuwalisha inakuwa si jambo la kutiliwa maanani kabisa. Utaratibu ni ule ule, kwamba chakula kinachopatikana kwa siku hiyo ndicho hicho hicho watakachopatiwa wanyama bila kujali kwamba wanyama watashiba au la.
Kwa mtindo huu wa ufugaji itakuwa ni ndoto kuona matunda yake, kama nilivyokwisha kusema katika makala zilizotangulia, kwa aina zote za mifugo, muda wa kumfuga mfugo hadi mavuno unajulikana.Lakini kwa mfumo huu wa ufugaji jambo la kufuga na kuvuna hapa inakuwa ni mpaka miaka na miaka ipite, kwa mfano, mnyama kama nguruwe anatakiwa avunwe ndani ya miezi sita tu, na hadi kufikia hapo, kama amefugwa kitaalam anatakiwa awe na nyama yenye uzito wa kilo sitini hadi themanini na sii chini ya hapo.
Tunaona jinsi ya kufuga na kuyafikia mafanikio hayo katika makala zinazofuata na shamba darasa litakuwepo ili tuweze kujifunza kwa vitendo, Sasa hapa chini tutaona FAIDA TANO TUTAKAZOPATA KAMA TUSIPOFUGA KWA MAZOEYA.
Faida ya kwanza kabisa ni Kupata faida kwa muda Mwafaka, katika mradi au Biashara yoyote, madhumuni ya kwanza kabisa ni kupata FAIDA, mafanikio chanya kwa mjasiriamali yeyote ndilo kusudi na haja ya moyo, hakuna mtu yeyote anaeanzisha mradi kwa kutegemea kuvuna hasara, hata mwizi anapojiandaa kwenda kuiba hujiandaa vyema, hata wakati mwngine hufanya sala au kwenda kwa mganga kufanya ulozi ili afanikiwe.Yaani AFAIDIKE kwa wizi wake.
Faida ya pili ni kutumia Gharama ndogo katika kuendesha mradi na kuyafikia matarajio yako kwa muda uliokusudia, unapokaa na mifugo yako kwa ufugaji wa mazoea usiofuata utaalam nakanuni ni dhahiri kuwa utafuga kwa muda mrefu, kufuga kwa muda mrefu ina maana utakuwa unawalisha wanyama wako kidogo kidogo ila kwa muda mrefu sana. hapa kuja kupata faida itakuwa kwa kusubiri sana
Faida ya tatu tutakayopata kama tusipo fuga kwa mazoea ni kujijengea heshima ya kuwa na boma bora litakaloheshimika kwa jamii inayotuzunguka au iliyombali. Hii maana yake ni nini?Kama ukifuga kitaalam maana yake mifugo yako itakuwa Bora na yenye afya njema, kwa maana hiyo kila mtu atataka kununua kutoka katika boma lako, kwa hiyo itakuwia rahisi kwako kufanya mauzo bila kuhangaikia sana soko, kuna msemo wa kiswahili tuliouzoea sana katika biashara, kwamba Kizuri chajiuza na Kibaya chajitembeza, Hutahitaji kujitangaza sana maana kazi hiyo watafanya wale walionunua kutoka kwako na kufaidi mazao ya boma lako.
Faida ya nne ni kuokoa muda, kufuga kitaalam kutaokoa muda wako na kukufanya uwe na muda wa kufuatilia mambo yako mengine, Kufuga kitaalam mojawapo ya msingi wake ni kuhakikisha unakuwa na bajeti inayotosheleza kuhudumia mradi kwa kipindi chote cha mradi wako, na bajeti ndiyo itakayoamua ukubwa wa mradi wenyewe, kwa habari ya bajeti hapa ndipo mfugaji anapotakiwa kutilia umakini kuliko mahali pengine popote.
Bajeti ni Kupanga, na kupanga ni kchagua, kwa maana ukubwa au udogo wa mradi utategemea ni nini kilichokuwa katika akaunti yako ya mradi, basi tuseme kuwa utaokoa muda wako kwa sababu tayari mahitaji yote katika mradi wako yatakuwa yanapatikana katika muda muafaka,basi hata muda wa kuhudumia mradi utakuwa mdogo maana matayarisho yote muhimu yatakuwa yameshaandaliwa
kwa muda mwafaka pi
Faida ya tano kwa kutaja kwa uchache tuu, maana faida za kufuga kwa Tija ziko nyingi zaidi ya tano, ila hapa tumeangazia kwa uchache tu, tutaendelea huko mbele zaidi kuona faida nyingine nyingi kadri tutakavyo kuwa tunasonga mbele, faida ya tano tutakayopata kwa kufuga kwa tija ni kuweza kuhifadhi MBEGU BORA kwa ajili ya kuendeleza boma lako la ufugaji, utakuwa ukijichagulia uzao ulio bara katika ama wanyama jike au madume, kumbuka hapa nimesema ama madume au majike, utatakiwa kuchagua upande mmoja tu kwa kukwepa kuzungusha kizazi kimoja kwa miaka mingi. Inashauriwa kuhifadhi majike zaidi kwa sababu ni rahisi kubadi madume kwa kuwa, kwa mfano kama ni ng'ombe, idadi ya madume watakao hitajika katika boma ni chache sana kulinganisha na majik. hivyo unashariwa kuchagua majike mengi zaidi.Madume utayanunua kutoka katika shamba lenye ubora kushinda la kwako.
Faida ya kutokuendeleza kizazi kimoja ziko nyingi, hatutaweza kujadili kwa mapana hapa maana hilo ni somo pana ambalo linahitaji muda na utaalam katika kulitolea maelezo. Kwa leo naomba tuishie hapa, ni Tumaini langu kuwa kuna kitu umepata katika makala yangu ya leo. Nakushukuru sana kwa kuyasoma makala haya mwanzo hadi mwisho, ni mategemeo yangu kuwa utatoa mani au ushauri wako hapo chini, comment chochote unachoweza kwa faida yangu na wengine na kwa Blog pia,
UBARIKIWE SANA.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Asante sana Mr John,
JibuFutaNaomba nikujibu kama ifuatavyo,
HYDROPONIC FODDERS TANZANIA ni kampuni inayotarajia kuanza hivi karibuni,madhumuni ya kuundwa kwa kampuni hii ni kumwezesha mfugaji kupata chakula cha mifugo yake kwa bei nafuu sana,chakula bora na kisafi.
Tutakuwa tunaandaa chakula kwa ajili ya ng'ombe,Nguruwe,Mbuzi na wanyama wote jamii ya Ndege.Katika makala zinazofuata nitaangazia juu ya ufugaji stadi wa wanyama jamii Ndege,
Nakushukuru sana kwa swali lako Bwana John.Endelea kufuatilia makala zinafuatia.