Karibu katika blog yetu tanze safari ya kufanikiwa na kuwa na uhuru wa kifedha

Jumapili, 23 Oktoba 2016

Faida za Kuwapa Wanyama tunaofuga Chakula Bora na Salama.

NG'OMBE WAPEWE MAJI SAFI NA SALAMA.
       Karibuni tena wana mtandao wetu pendwa, ni matumaini yangu kuwa wote ni wazima na mnaendelea na majukumu ya kila inapoitwa leo, ilimradi maisha yetu yanasonga mbele kama ambavyo tumejiwekea malengo yetu, na tunapambana tuyafikie malengo yenyewe. Katika makala moja iliyotangulia niliangazia umuhimu wa kufuata KANUNI, sasa leo naomba tujaribu kupitia japo kwa ufupi kipengele kimoja muhimu sana katika tasnia ya ufugaji kwa ujumla.
      Tunaposema chakula Safi, bora na Salama tunamaanisha nini? Tukirudi nyuma tuliona baadhi ya wafugaji wamezoea kufuga kwa mazoea, kufuga huku kwa mazoea ndiko kunakofanya wafugaji wengi kuangukia katika kulisha wanyama wao chakula kisichokuwa safi bora na salama. Kulisha wanyama chakula cha aina hiyo kuna madhara makubwa katika afya ya wanyama wenyewe na binadamu watakaotumia mazao yanatayopatiana tokana na wanyama hao. Ndio maana kwa mfano inakuawa vigumu sana kuafanya biashara ya mazao ya wanyama baina ya nchi na nchi, hii ni kwa sababu tunalisha wanyama vyakula visivyokidhi viwango.
       Kuna hasara nyingi zinazotokea tunapowapa wanyama wetu chakula kisicho safi bora na salama, na kuna faida nyingi sana tunapowapa wanyama wetu chakula safi bora na salama.Tuanze kuangazia hasara zinazotokea tunapowapa wanyama wetu chakula kibovu Wanyama kama walivyo hawana tofauti yoyote katika uhitaji wa chakula safi na bora na salama ,sisi wanadamu tumewapita kwa kuwa na utashi tu. Zipo hasara nyingi zinazotokana na kuwapa mifugo yetu chakula kisicho safi na salama.
       Hasara ya kwanza kabisa ni kutokupata faida tokana ufugaji wetu, madhumuni ya mfugaji yeyote ni kupata faida katika kazi yake ufugaji, ikiwa ni pamoja na mifugo yake kuzaa na kuongezeka, hasara nyingine ni kupoteza muda kuanasababisha kutokufikia malengo katika muda tulijiwekea, hii inasababisha kuyumba sana kwa malengo tuliyojiwekea, kwa mfano unaweza kuanza mradi wa ufugaji kwa ajili ya kujipatia pesa kwa ajili ya kulipia ada za watoto wako, unatumia pesa kwa kuanzisha mradi wa kufuga ng'ombe wa maziwa, mtaalam wako wa mradi anakushauri labda badala ya kununua ndama jike watano, ununue mitamba wawili wenye mimba tayari, atakushauri labda ununue walio na mimba ya miezi mitatu, ili baada ya miezi sita wapate kuzaa, maana hapo utakuwa sasa na ng'ombe wanne, idadi inayokaribia na idadi ya ng'ombe uliyokusudia kununua hapo awali, lakini wawili watakuwa wanaanza kukulipa mapema ilhali hao wadogo wanapanda taratibu kuukuza mradi.
          Sasa tuangazie hapa hasara inapatikana vipi kwa kuwalisha ng'ombe wako chakula kisicho safi bora  salama .Itakuwa vizuri kwanza tukajua chakula Bora Safi naSalama ni chakula cha aina gani? Chakula bora safi na salama ni chakula ambacho kimeandaliwa kutoka vyanzo salama, mahali  salama na vilivyochanganywa kwa mizania iliyo sawa, hapa tutaangalia kipengele kimoja baada ya kingine.
          Vyanzo salama ni nini maana yake ?kwa mfano tuangalie majani yaliyozoeleka kwa kila mtu kwamba ni chakula kikuu cha ng'ombe, majani utakayotumia kulisha ng'ombe wako yanapatikana kutoka wapi? Pengine umemtuma kijana wako wa kazi, katika hangaika yake akazifuma nyasi mahali pembeni ya barabara, kumbe jana yake eneo hilo paliharikia gari, majani yakachafuliwa aidha kwa kumwagikiwa na maji ya betri, petroli,dizel , oil au girisi,  majani yale yakaletwa mojakwa moja zizini na kuwalisha ng'ombe wako, ni dhahiri kuwa majani hayo hayana ubora uanaotakiwa. sii safi wala salama.
          Ili ng'ombe akue mwenye afya njema hapaswi kupewa majani peke yake, anatakiwa kupewa
chakula chenye virutubitusho vyote, sasa tuangazie hivi virutubisho,  kwa mfano kunahitajika mchanganyiko wa pumba, mashudu ya alizeti,mashudu ya pamba, chumvichumvi maalum yenye madini muhumu, polad,na vitu vingine vingi, vitu vyote hivi vinatakiwa viwe salama na safi, kwa mfano pumba inaweza kuwa imetokana na mahindi yaliyokuwa yamewekwa sumu ya kuhifadhia mahindi, kwa vyovyote pumba hii itakuwa sii salama kwa ng'ombe wako, hali kadhalka mashudu yanaweza kuwa hayakuhifadhiwa sehemu salama baada ya kukamuliwa mafuta, yakawa yamemwagwa chini na kuchafuliwa na vitu kama sumu na takataka nyingine hatari kwa ng'ombe wako.
         Unapowapa wanyama wako vyakula kama hivi usitarajie kuwa watakuzalia matunda kama ulivyotarajia, tutakuwa tunafanya yaleyale ya kufuga kwa mazoea. Ili kukamilisha mlo kamili wa wanyama tunaowafuga ni lazima tuwapatie maji safi na salama, tena maji yawe ya kutosha,hapo awali nilisema kwamba wanyama wako sawasawa na sisi, wamepungukiwa na utashi tuu, sasa utakuta mfugaji anajichotea maji toka chanzo chochote na kuwapa wanyama wake, tena maji kidogo,bila kujiridhisha kwamba wanayama wamekunywa maji na kutosheka, na kuwa pia wanapatiwa maji salama ya kutosha mara kwa mara.
          Nasisitiza mara kwa mara kwa sababu katika kufuga kwetu kwa mazoea unaweza kukuta mfugaji anawapa mifugo yake maji hata wakati mwingine mara mbili kwa wiki, hii si sawa kabisa!
maji safi na salama ni kitu muhimu kabisa. Kuwapa wanyama wako chakula cha kutosha halafu usiwepe maji ya kutosha utakuwa unafanya kazi bure,itakuwa vigumu kufikia malengo yako.
        Katika bonda la kufugia wanyama wako, hori la kulia chakula ni lazima linakuwepo, sambamba na hori hilo, pembeni pawepo na chombo cha kuwekea maji pia, ili mnyama apate kupoza kiu yake mara anapojisikia kiu.Ng'ombe anayekamuliwa maziwa maji salama na kutosha ni muhimu sana kwake ili uweze kupata maziwa ya kutosha.
     Kuna faida nyingi zinazopatikana tunapowapa  wanyama wetu chakula cha  kutosha, yaani wanyama wale na kushiba kila siku, faida ya kwanza ni pamoja  kupata matunda mengi ya kutosha, kwa mfano Maziwa, Nyama, Mayai pamoja na Mbolea ya kutosha tutakayotumia katika kilimo ili kujiongezea kipato zaidi. Faida nyingine  ni kujijengea heshima katika soko, kwa vyovyote kama unawalisha vizuri ng'ombe wako, ni dhahiri kuwa watakupatia maziwa bora na matamu, mtu anaponunua kwako na kugundua ubora wake ni wazi kabisa kwamba atakuwa ana nunua maziwa toka shambani kwako kila siku,tena atawatangazia na watu wengine.
     Kwa kulisha mifugo yako chakula bora na salama mifugo yako itakuwa na afya bora, hivyo kufanya wanyama wako kuwa na miili mikubwa na yenye kuvutia, hapa utakuwa umesha jijengea brand yako ya wanyama, wawe ng'ombe, mbuzi, nguruwe ama wanyama jamii ndege, sifa ya kuwa na brand bora itakufanya  ujulikane haraka na baada ya muda utakuwa unafanya biashara kubwa bila kuhitaji ghrama ya kufanya matangazo.
      Katika makala haya nimeangazia baadhi ya vipengele muhimu kwa juu juu tu, katika makala zinzofuata tutaanagazia kwa undani zaidi, tutaangazia kwa vipimo pia, kwa mfano ng'ombe nahitaji maji lita ngapi kwa siku, majani kilo ngapi na kadhalka, kwa hiyo nawakarisha katika makala zinazofuta, karibuni sana.
      Nikushukuru sana wewe uliyesoma makala haya mwanzo hadi mwisho, nakuomba sana uache maoni yako hapo chini, ni muhimu sana kuacha maoni au maswali au marekebisho ili niweze kufanya tathmini ya maandiko haya.
    BWANA MUNGU AKUBARIKI SANA.

Maoni 1 :

  1. Nimefurahishwa sana n makala hii kwani mimi nimfugaji wa ngombe tena kijijini mwanga Kilimanjaro nashukuru kwa kujua jinsi ninavyopaswa kuwahudumia ngombe wangu na si kwa kuwapa majani tu bali ni muhimu kuwapa virutubisho maalum kama Poland,mashudu nk sasa ninasubiri kwa hamu kujua zaidi hasa vipimo wakati ngombe akiwa ananyonysha na wakati hanyonyeshi ili kufanya zaidi kibiashara na kufanikiwa sana ubarikiwe

    JibuFuta