Nimewahi kusoma na kusikia toka kwa watu wengi waliofanikiwa, hata leo asubuhi nimesoma makala moja katika gazeti la leo la Raia mwema, ukurasa wa 26, kichwa cha habari"Kutoka shilingi elfu NNE hadi bilionea" Jambo hili linatia moyo sana, kwamba ili mtu ufanikiwe sii lazima uanze na mtaji wa malaki au mamilioni, kiasi kidogo kilichopo ndicho hicho hicho cha kuanzia, na matokeo yataanza kuonekana kadri siku zinavyosonga mbele,
Hali ya maisha imekuwa ngumu na inaendelea kuwa ngumu kadri siku zinavyosogea, watu wa mjini wamezoea kusema jana ni afadhali kuliko leo, lakini kauli hii haipaswi kupewa nafasi katika maisha yetu, katika jukwaa hili tutaangazia namna ya kuufanya huu msemo usomeke kinyume chake, yaani tutamke kuwa siku ya leo ni nzuri kuliko jana ilivyokuwa,
Jambo hili lawezekana bila kikwazo chochote, nawakarisha wote mtakaofanikiwa kulifikia jukwaa hili tuanze safari ya matumaini pamoja, safari ambayo naamini tutafanikiwa kuwasili salama katika uhuru wa kifedha ,uhuru ambao tulio wengi bado tuu katika utumwa huu mbaya kuliko aina nyingine zote za utumwa, watu wote waliokwisha funguliwa katika aina hii ya utumwa utawajua tu kwa tabia zao, kwamba ni waangalifu na waaminifu sana katika matumizi ya fedha zao, maana kamwe hawataki tena kurudi utumwani. Karibuni sana mtandaoni na Bwana Mungu atutangulie katika safari yetu hii.
Nakushukuru kwa kusoma makala haya,naomba ushauri wako,pia naomba unikosoe pale ambapo sijaandika vizuri.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni