Karibu katika blog yetu tanze safari ya kufanikiwa na kuwa na uhuru wa kifedha

Jumatano, 12 Oktoba 2016

Umuhimu wa kufuata kanuni za ufugaji.

            Kanuni ni utaratibu maalum unaofuatwa katika kufikia mafanikio katika mipango tuliojiwekea, bila kufuata kanuni kikamilifu ni vigumu kufikia mafanikio chanya, mradi wowote unaofuata kanuni, mafanikio ni lazima, kwa mfano tuangalie jambo moja dogo, mama anapotaka kupika ugali ,anafanya maandalizi ,unga utakuwa kitu cha kwanza kuwaza, itafuatia matayarisho ya kitoweo cha kutowezea ugali, tumezoea kusema ni mboga ya kulia ugali, hapa sasa mama ataanza kufanya mapishi yake.   Kuhusu mboga mama atajua mwenyewe jinsi atakavyo andaa.  Lakini mimi nataka tuangazie kanuni za kufuata katika kupika ugali,
          Mama atakuwa na unga,sufuria na maji,  pia moto utahitajika kwa kupikia uagali wenyewe, hapa kanuni isipofuatwa,kuna uwezekano ugali usipatikane, kwa mfano, mama akatenga maji kipimo anachotaka, na unga pia halafu akaamua kusonga kwanza ugali kabla ya kubandika kwanza maji jikoni yachemke ndio asonge ugali, hata ausonge mwezi mzima kwa moto wa gesi,  ugali huo hautaiva daima, shida hapa ni kutokufuata kanuni ya ksonga ugali.   Sote tunajua utaratibu au kanuni ya kusonga ugali nayoni hii, washa moto, bandika au injika maji jikoni, chochea moto hadi maji yachemke kwa dakika tano, ongeza unga kiwango kadiri ya maji yenyewe, songa ugali wako,dakika kumi ni nyingi, ugali unaanza kunukia, ugali unakuwa tayari umeiva, ni wa kuipuliwa tayari kwa kutengwa mezani,
      Hapa kanuni ya kusonga ugali inakuwa imefuatwa tofauti na hapo juu.   Kama tulivyoangazia katika makala ya jana,  tulijadili kwa kifupi faida za kutumia kanuni katika ufugaji, kabla ya kuanza kufanya mradi ni lazima kufanya upembuzi yakinifu, unaubuni mradi wako katika mawazo, kisha unauweka katika maandishi, (daftari maalum ambalo utakuwa urekodi taarifa zako zote ni muhimu sana)
       Kiasi cha pesa (MTAJI)utakacho kuwa nacho ndiyo DIRA hasa ya kukupeleka kule unakotaka kwenda, chukulia mfano wa mtu anaetaka kusafiri, kipimo cha kwanza ni kutathmini umbali anaotaka kusafiri, umbali huo ndio ndio utakaozaa nauli atakayo lipa, na maandalizi ya mradi wako ni hivyo hivyo, kwamba kiasi cha fedha(MTAJI)ndio utakao kuongoza kufanya tathmini ya mradi wako.   Mara nyingi hapa ndipo watu hufanya makosa makubwa, kufanya mahesabu kwenye calculator na kuona matokeo mazuri, kwa mfano unajipa moyo kuwa utaanza na ng'ombe watano, chukulia kwa mfano watakamuliwa lita 40 kila mmoja, (5x40 )unapata lita 200, utauza kila lita moja shilingi 2000  kwa siku utatengeneza shilingi laki nne, laki nne , kwa mwezi utapata shilingi milioni kumi na mbili, hapa moyo unadunda kwa furaha kubwa, utakuwa unajidanganya, mahesabu ya namna hii bila kufanya upembuzi yakinifu mbele ni anguko kubwa.
       Mimi binafsi yalishanikuta haya majanga. Kimsingi mradi wowote unahitaji kujipanga, kwa kufanya maandalizi yote kuanzia katika kuuwaza mradi wenyewe, kufanya upembuzi yakinifu, kupata ushauri kwa wataalam wa mambo ya ufugaji, kutembelea mashamba yanayofanya vizuri katika ufugaji, huko utajonea mwenyewe kwa macho, utauliza maswali, kwa mfono ni namna gani utakavyoweza kupunguza gharama za ufugaji huku ukipata mafaniki chanya.
         Katika makala zinazofuatia tutaangazia kwa mapana na mrefu jinsi kufanya ufugaji kitaalam na kutengeneza pesa za kujikimu kuendesha maisha yetu kwa uhuru na kuyafurahia.
        Nakushukuru kwa kusoma makala haya,naomba ushauri na pia unikosoe pale nilipokosea.


Kwa jambo lolote,kuwa huru kuwasiliana nami katika njia zifuatazo:
    E-mail: nkuus2001@yahoo.com,
                anael.ludovick6@gmail.com,
                +255714440554.

Maoni 1 :

  1. Usichanganye vitu,ikitska kuongelea mifugo,iendane na mifano yakeHeading inaongelea mifugo,habari nzima ime base kwenye kusonga ugali.good start.

    JibuFuta