Nimejaribu kuzungumza na baadhi ya wafugaji katika maeneo mbalimbali katika jiji la Dar es salaam na kubaini kilio chao ni cha aina moja, kwamba gharama za kulisha mifugo kama ng'ombe,nguruwe, kuku na mbuzi nk, ziko juu sana, huku faida inayopatikana baada ya mauzo kuwa ni ndogo au wakati mwingine faida kutoonekana kabisa, nilipojaribu kufanya madodoso nikabaini makosa yanayofanywa na baadhi ya wafugaji yanafanana kwa karibu sana, nikagundua tatizo lililokuwa kubwa zaidi ni lile la kulisha mifugo kwa muda mrefu kabla ya kupelekwa sokoni, ukisoma katika miongozo mbalimbali utakuta imebaishwa muda kamili wa kufuga mfugo kuanzia siku ya kwanza hadi siku ya kuvuna mfugo wenyewe, tutaona katika makala zijazo.
Wataalamu wamebainisha katika makala mbalimbali kanuni za ufugaji, na kanuni hizi zinakuwa zimethitishwa kitaalam, na pale mfugaji anapozifuata bila kukosea, matokeo kwa namna yoyote lazima yawe mazuri na ya kutia moyo, hii ikiwa ni pomoja na kuanza ufugaji kwa kuchagua mbegu bora kutoka vyanzo vilivyopendekezwa, kujenga mabanda bora na kwa kutumia ramani zilizopendekezwa na wataalam wa mifugo, mifugo kupatiwa chanjo katika utaratibu uliopendekezwa na pia chanjo zenyewe zipatikane katika maduka yaliyopendekezwa.Imegundulika kuwa kuna wafanya biashara wasio waaminifu wanaouza chanjo zisizokuwa na ubora, zilizopitwa na wakati au zisizo thibitishwa na wakala wa serikalali wa mdawa na chanjo, hivyo utakuta mfugaji amefuata ratiba kamili ya chanjo lakini wanyama wanashambuliwa na magonjwa yaliyopatiwa chanjo zake. kwa vyovyote vile hapa lazima mfugaji atapiga hatua kurudi nyuma badala ya kusonga mble kimaendeleo, Ieleweke hapa kuwa ili kufikia malengo tuliyojiwekea ni lazima kanuni zote za ufugaji zifuatwe bila kuruka hata kipengele kimoja.
Kumekuwa na tabia ya wafugaji kufuga kwa MAZOEA, yaani bila kufuata kanuni zilizopendekezwa au kutafuta ushauri kutoka kwa wafugaji wenzao wanaofuga kwa mazoea kama wao, mara nyingi hili hutokea ama kwa kutafuta ufumbuzi kwa gharama ndogo au kutokujua, utakuta mfugaji anao mtaji mkubwa wa kutosha, lakini ukitembelea mradi wake utakuta uko kinyume kabisa na gharama alizogharamia.
Katika makala zinazofuata tutaona mpangilio kamili wa jinsi ya kuanzisha mradi wa ufugaji kwa kutumia kanuni zilizopendekezwa na matunda yataonekana bila tatizo lolote, kutakuwa na shamba darasa hapa Dar es salaam eneo la Madale ambapo kutakuwa na utaratibu maalum wa kutembelea mradi na kujifunza kwa vitendo. Jambo kubwa na la msingi katika ufugaji ni malisho bora, nasema hili ni kubwa na la msingi kwa sababu hata kama utazingatia mambo mengine yote kwa usahihi kabisa halafu mifugo isipate chakula bora na cha kutosha, utakuwa unafanya kazi bure, mara nyingi mnyama yeyote hujitambulisha kutokana na jinsi anavyolishwa chakula, hapa hapahitajiki mtambo wowote wa kubaini jambo hili, mnyama anaefugwa kwa kupatiwa mahitaji yote sahihi utamjua kwa afya yake, kama ni ng'ombe wa maziwa ukimchunguza hata kwa kuona kiwele chake utajua kweli huyu mfugaji ni hodari, na anapata maziwa mengi ya kutosha, utakuta wakati mwingine ng'ombe wa maziwa amekonda mifupa inaonekana hata mbavu zinahesabika, hata maziwa yanayokamuliwa kutoka ng'ombe huyu yanakuwa ya kutiliwa mashaka.
Katika makala zinazofuata tutaangazia jinsi ya kupitia harakati zote hizi kwa gharama nafuu kwa upande wa hili kubwa la malisho bora na ya uhakika, kwenye upande wa madawa hakuna njia ya kukwepa gharama, maana tutaangukia hukohuko kama tulivyozungumzia hapo juu, hili la madawa lazima tuyapate kutoka katika vyanzo salama na vya kuaminika,
Tukutane tena katika makala ya kesho tutembee hatua kwa hatua kuelekea kwenye mafanikio katika ufugaji bora na wa kisasa na wenye tija.
Nakushuru sana sana kwa kusoma makala haya, kama kuna maswali au maoni, tafadhali sana usiache kuandika maoni yako katika sehemu ya kuandikia maoni hapo chini. karibu katika mapambano.
Asante sana Mr John,
JibuFutaNaomba nikujibu kama ifuatavyo,
HYDROPONIC FODDERS TANZANIA ni kampuni inayotarajia kuanza hivi karibuni,madhumuni ya kuundwa kwa kampuni hii ni kumwezesha mfugaji kupata chakula cha mifugo yake kwa bei nafuu sana,chakula bora na kisafi.
Tutakuwa tunaandaa chakula kwa ajili ya ng'ombe,Nguruwe,Mbuzi na wanyama wote jamii ya Ndege.Katika makala zinazofuata nitaangazia juu ya ufugaji stadi wa wanyama jamii Ndege,
Nakushukuru sana kwa swali lako Bwana John.Endelea kufuatilia makala zinafuatia.